Loading...

BOB WINE ATANGAZA VITA NA MUSEVENI, AWEKA BAYANA MPANGO WA KUMNG'OA IKULU

Loading...
Mbunge wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarurufu kama Bobi Wine, amefichua kuwa atawania kiti cha urais nchini humo mwaka wa 2021 kwa matumaini ya kumaliza utawala wa miongo mitatu wa Rais Yoweri Museveni.

Mbunge huyo wa upinzani amekuwa akishinikiza kustaafu kwa Museveni ili kutoa nafasi kwa viongozi wachanga.

Wengi wanaamini kuwa huenda Wine anajiandaa kukabiliana na Museveni kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kulingana na jarida la Observer, Wine alinukuliwa akisema kuwa njia ya haraka ya kumwondoa Museveni madarakani ni kupitia kura wala sio kupitia njia nyingine.

Wine alisema hatatumia vita kama njia ya kupata madaraka na kupendelea jinsi Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammen alivyopokonywa madaraka baada ya kuliongoza taifa hilo kwa miongo miwili. 

Wine alisemekana kuchukua nafasi ya hasimu mkuu wa Museveni, Kizza Besigye, ambaye ndiye kiongozi maarufu zaidi wa upinzani nchini humo.

Serikali ya Museveni imejaribu kuzima juhudi za mbunge huyo mchanga aiwe na ushawishi kwa umma kwa kumkamata, kumzuilia na kumtesa, lakini matukio hayo yamechangia kumfanya kuwa maarufu zaidi.
Na Said Hussein.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BOB WINE ATANGAZA VITA NA MUSEVENI, AWEKA BAYANA MPANGO WA KUMNG'OA IKULU BOB WINE ATANGAZA VITA NA MUSEVENI, AWEKA BAYANA MPANGO WA KUMNG'OA IKULU Reviewed by By News Reporter on 1/03/2019 11:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.