Loading...
Mwaka unapoanza watu wengi huwa tunakuwa na msisimko mkubwa wa kutengeneza malengo yanayogusa sehemu mbalimbali za maisha yetu lakini kwa mbaya sana wengi huishia kuweka malengo hayo bila kuchukua hatua zozote kuyatekeleza.
Baadhi ya sababu ambazo huwa zinawakwamisha wengi ni hofu, kutojiamini, kusubiri muda sahihi, kuogopa maoni ya watu na fikra za kukosa muda. Tumesema mwaka huu ni wa tofauti kwetu na ni mwaka wa kuandika historia mpya, sababu hizi si za msingi na hazipaswi kutuzuia kutekeleza malengo yetu.
Imarisha uwezo wako wa kuchukua hatua kwa vitendo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1. Kuwa na uthubutu wa kujaribu, usiogope kujaribu jambo jipya.
2. Usisubiri mambo yote yakae sawa,hakuna siku kila kitu kitakaa sawa.
3. Kuwa na ujasiri wa kufanya kile unachokiogopa, ukishaanza kukifanya tu hofu yote inapotea.
4. Anza leo , usiruhusu kusema utaanza kesho au wiki ijayo. Kufanya hivyo unakaribisha kushindwa.
5. Usitumie muda mwingi sana kujiandaa kufanya jambo, anza hivyo hivyo kwa kutumia hicho hicho ulichonacho.
6. Usiogope watu wengine watasema nini au watakuonaje. Kama unaamini katika malengo yako na kwamba unachokifanya ni sahihi usihitaji kibali cha mtu mwingine.
Kuwa na mawazo na mipango mizuri pekee haikusaidii kubadili maisha yako, ni lazima uchukue hatua kwa vitendo kutekeleza mipango hiyo ili mambo yaweze kubadilika.
Na Richard Daudi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

CHUKUA HATUA SIKU ZISHAANZA KUSOGEA, KUJIWEKEA MALENGO PEKEE HAITOSHI
Reviewed by By News Reporter
on
1/03/2019 10:49:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: