Loading...
Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Rarua rarua’ na 'Sare' Malaika amefunguka na kuweka wazi sababu iliyomfanya mpaka akapotea kwenye gemu.
Malaika amesema kuwa ameamua kukaa kimya kwa muda mrefu ili kuangalia upepo wa gemu unaendaje kwani gemu inabadilika kila siku.
Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao mmoja wa habari, Malaika alisema kuwa anajua mashabiki wake wanajiuliza kwa nini hasikiki tena kwenye muziki lakini ukweli ni kwamba yupo anaangalia njia nzuri ya kuwafurahisha mashabiki wake.
"Japokuwa nasafiri huku na kule lakini yote hiyo ni kuangalia upepo wa muziki unavyokwenda na ni kitu gani mashabiki wanakitaka kwa hivi sasa kama ni Singeli, Mduara au miondoko mingine yoyote ili niweze kutoka tofauti".
Na Hamadi Ramadhani.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MALAIKA AFUNGUKIA UKIMYA WAKE
Reviewed by By News Reporter
on
2/11/2019 11:20:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: