Loading...

MUSEVENI AIDHINISHWA KUONGOZA UGANDA MAISHA YOTE

Loading...
Kamati kuu ya utendaji ya chama kinachotawala nchini Uganda, National resistance movement NRM, imemuidhinisha rais wa sasa Yoweri Museveni kuwania urais mwaka 2021 na katika chaguzi zitakazofuatia kwa mda wa miaka 50 ijayo.

Uamuzi huo ulifikiwa wakati wa kufunga kikao maalum cha viongozi wakuu wa chama cha NRM kilichofanyika katika Wilaya ya Nwoya baada ya muswada uliyowasilishwa na kiranja wa serikali Ruth Nankabirwa na kukubaliwa na kamati nzima.

Kwa mujibu wa maamuzi ya kamati ya juu ya chama cha NRM, namba 1(g), viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho ambacho kimetawala Uganda tangu mwaka 1986, wamemuidhinisha Museveni kuitawala Uganda maisha yake yote.

SABABU ZA MSINGI NRM KUFANYA UAMUZI HUO

Wamemtaja kama kiongozi shupavu na Jenerali katika ukombozi wa Bara la Afrika, mwenye uwezo wa kuleta maendeleo ya kudumu, sio tu kwa Uganda na Jumuiya ya Afrika Mashariki pekee, bali katika bara la Afrika kwa jumla.

MAREKEBISHO YA KATIBA

Kulingana na katiba ya Uganda, Museveni anaruhusiwa kuwania urais bila kizuizi chochote, baada ya bunge kufanyia katiba marekebisho na kuondoa kizuizi cha umri kwa wagombea wa urais, mwaka 2017.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MUSEVENI AIDHINISHWA KUONGOZA UGANDA MAISHA YOTE MUSEVENI AIDHINISHWA KUONGOZA UGANDA MAISHA YOTE Reviewed by GEOFREY MASHEL on 2/21/2019 08:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.