Loading...
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hataruhusu mwanamke hata mmoja kutoka nchini humo kuonyesha mwili wake kwa umma kama njia moja ya kuwavutia watalii.
Akiwa kwenye mkutano na wawekezaji katika Ikulu Alhamisi Februari 7, Museveni alilaani pendekezo hilo la kutaka kuwatumia wanawake wenye makalio makubwa kama kivutio cha utalii.
Museveni alidai kuwa pendekezo hilo lililotolewa na waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda halikuwa limejadiliwa na baraza la mawaziri.
Aidha, Rais Museveni pia alisema hakuna uhakika kwamba wanawake kuonyesha makalio yao itavutia watalii Uganda.
"Huu haukuwa uamuzi wa baraza la mawaziri, watu hawapaswi kuja hapa kuona wanawake, sijafurahishwa na pendekezo hilo hata kidogo. Hiyo ni kama kuwauza wanawake wetu kwa watalii," Museveni alisema.
Museveni pia aliasema wanawake wanapaswa kuheshimiwa na kushughulikiwa ipasavyo ila sio kuwaanika mitandaoni kama njia moja ya kuwauza.
"Lazima tujipe muda wa kujadili suala hili, niko na maoni yangu binafsi na tayari nishayazungumzia, siwezi wakubali wajukuu wangu kuonyesha miili yao kwa umma eti kwa ajili ya kukuza utalii, ningependa tumtumie Abenakyo, Miss World Africa kuuza Uganda kwa mataifa mengine," Museveni aliongezea.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MUSEVENI APINGA PENDEKEZO LA KUWATUMIA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA KAMA KIVUTUO CHA UTALII
Reviewed by By News Reporter
on
2/10/2019 10:12:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: