Loading...

NABII OWUOR WA KENYA AJITABIRIA MAKUBWA, AJIFANANISHA NA YESU

Loading...
Nabii maarufu David Owuor ametabiri jinsi atakavyoondoka humu duniani baada ya kukamilisha kazi aliyotumwa kufanya na Mungu.

Owuor ambaye anafanya shughuli zake za unabii nchini Kenya, hujitaja kuwa nabii mwenye nguvu zaidi ulimwenguni alisema ataondoka humu duniani jinsi Yesu alivyoondoka. 

Akitoa unabii kwa wafuasi wake katika kanisa la Repentance and Holiness Ministry, Owuor alisema alikutana na Mungunu mawinguni na akamuelezea habari za kufariki kwake. 

Kulingana na Owuor, atauawa katika mji wa Yerusalemu na mwili wake hautazikwa ila baada ya siku 3 atafufuka na kuenda mbinguni kukutana na Mungu. 

"Baba yangu na Mungu wangu amezungumza nami, alianza kuzungumza nami akiwa mwenye furaha kuu, aliniambia kwamba nitauawa pindi nitakapokamilisha kazi yake," Owuori alisema.

"Nitakufa kwa siku 3 na baada ya hapo nitafufuka na Mungu atanichukua kwenda mbinguni kulingana na kitabu cha Ufunuo 11:7.1," Owuor aliongezea. 

"Nitauawa baada ya kumaliza kufanya kazi ya Mungu, sitazikwa na kwa siku ya 3 Mungu atanichukua kwenda mbinguni, nitauawa Yerusalemu na hii sio mara ya kwanza mimi kuzungumza na Mungu, " Owuor aliongezea. 

Nabii Owuor alisema kuwa alikutana na Mungu mawinguni ambapo alimueleza habari ya kifo chake.
Na George Owino.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NABII OWUOR WA KENYA AJITABIRIA MAKUBWA, AJIFANANISHA NA YESU NABII OWUOR WA KENYA AJITABIRIA MAKUBWA, AJIFANANISHA NA YESU Reviewed by By News Reporter on 2/10/2019 10:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.