Loading...
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameionya Marekani kuhusiana na makombora ya nchi hiyo barani Ulaya.
Akizungumza na Bunge la huko Moscow, Putin amesema kuwa kuwepo kwa makombora ya Marekani barani Ulaya - yenye uwezo wa kuipiga Moscow kwa dakika 10 - ni tishio kwa usalama wa nchi ya Urusi.
Putin ameongeza kwa kusema kuwa Urusi haitokuwa ya kwanza kupeleka makombora yake barani Ulaya lakini hatua kama hiyo kutoka kwa Marekani kutailazimisha Urusi kufanya hivyo hali amabayo itahatarisha usalama wa kimataifa.
"Tunahitaji kuchukua hatua za kutosha katika suala hili, "alisema Putin.
"Urusi italazimika kuunda na kupeleka silaha ambazo zinaweza kufikia sio tu maeneo ambayo tutakuwa na tishio nayo moja kwa moja," aliongeza, "lakini pia maeneo ambayo kuna vituo vya kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya mifumo ya makombora inayotishia sisi. "
Putin pia ametangaza maendeleo ya kombora mpya ya hypersonic - Zirkon - yenye uwezo wa kusafiri mara tano kasi ya sauti na ambayo inaweza kufyatuliwa kutoka kwenye nyambizi.

Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS WA URUSI 'PUTIN' AICHIMBA MKWARA MZITO MAREKANI
Reviewed by By News Reporter
on
2/21/2019 09:30:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: