Loading...

115 WAPOTEZA UHAI KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI MALI

Loading...
Watu 115 wa kabila la Fulani wameuawa baada ya kuzuka mapigano ya kikabila nchini Mali.

Kiongozi wa taasisi ya  Fulani  Tabital Pulaaku,Abdulaziz Diallo, alisema kutokana na shambulizi lililofanywa na wafuasi wa kundi la Dogon mida ya asubuhi katika kijiji cha  Egossagou watu 115 wamepoteza maisha.

Katika shambulizi hilo mwenyekiti wa kijiji cha Egossagou  na wajukuu zake pia waliuawa.

Wafuasi wa kundi la Dogon  wanawashutumu kabila la Fulani kwa kushirikiana na makundi ya kigaidi yaliyopo kaskazini mwa nchi hio.

Kabila la Fulani linaloishi katikati mwa nchi ya mali ambao wanajishughulisha na shughuli za ufugaji limekuwa likishambuliwa mara kwa mara miaka ya hivi karibuni kutokana na mashambulizi ya kigaidi katika eneo hilo.
Na Richard Mtweve.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
115 WAPOTEZA UHAI KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI MALI 115 WAPOTEZA UHAI KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI MALI Reviewed by By News Reporter on 3/25/2019 07:27:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.