Loading...

DHORUBA YA IDAI YAUA ZAIDI YA WATU 700, MILIONI MOJA WAATHIRIWA

Loading...
Watu wasiopungua 700 wameripotiwa  kufariki kufuatia dhoruba kali iliotokea  nchini Msumbiji, Malawi  na Zimbabwe.

Mvua kali na upepo  iliosababisha  mafuriko nchini imepelekea maafa makubwa katika mataifa hayo  katika ukanda wa Afrika Kusini.

Waziri wa  mazingira wa Msumbiji Celso Correira amefahamisha kuwa watu 417 wamefariki kutokana na dhoruba kali hiyo ya Idai.

Watu waliofariki nchini Zimbabwe imefahamishwa kuwa watu 259 huku nchini Malawi ikitangazwa kuwa watu 56 pekee ndio waliofariki.

Shughuli za uokoaji bado zinaendelea  huku  mlipuko wa kipindupindu umeripotiwa katika ameneo yalioathirika na dhoruba hiyo ya Idai.

Watu zaidi ya  milioin 1 na nusu wakiwemo watoto wameathirika na dhoruba hiyo iliotokea wiki iliopita nchini Msumbiji, malawi na Zimbabwe.

Rais wa Msumbiji Filipi Nyusi alitangaza  siku tatu za maombolezo  nchini humo kufuati maafa yaliotokea kufuatia  dhoruba hiyo.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DHORUBA YA IDAI YAUA ZAIDI YA WATU 700, MILIONI MOJA WAATHIRIWA DHORUBA YA IDAI YAUA ZAIDI YA WATU 700, MILIONI MOJA WAATHIRIWA Reviewed by By News Reporter on 3/25/2019 07:13:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.