Loading...
Waziri mkuu wa India Narendra Modi amesema hii leo kwamba India imeiharibu satelaiti iliyokuwa ikitembea katika anga za chini katika jaribio lake la kombora ambalo linalifanya taifa hilo kuwa miongoni mwa mataifa makubwa yenye teknolojia ya anga.
India inakuwa nchi ya nne baada ya Marekani, Urusi na China kufanya jaribio kama hilo.
Waziri wa fedha wa India Arun Jaitley amesema mbele ya mkutano na waandishi wa habari kwamba, hili si jaribio linalolenga kutishia taifa jingine lolote.
Katika hotuba ya nadra kwa njia ya televisheni na wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu Modi amesema wanasayansi wa India wameiangusha satelaiti hiyo iliyokuwa umbali wa kilomita 300 na kuongeza kuwa huu ni wakati wa kujivunia kwa India.

Na Rehema Jafari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
INDIA YASHIKA NAFASI YA NNE KWA UWEZO WA SILAHA
Reviewed by By News Reporter
on
3/28/2019 09:00:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: