Loading...
Burundi imewaachilia huru wanafunzi watatu wa kike ambao walikamatwa wakishutumiwa kuichafua kwa kuichorachora picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vyao vya shule. Waziri wa sheria Aimée Laurentine Kanyana ameeleza.
Kushikiliwa kwa wasichana hao takribani majuma mawili yaliyopita kwa shutuma za kumtusi rais kulizusha kampeni mitandaoni za kutaka wasichana hao waachiliwe kampeni iliyokua na jina #FreeOurGirls, watu wakituma picha kwenye mitandao ya Twitter.
Waziri amesema wasichana hao wenye miaka 15,16 na 17 wameachiwa huru kwa muda.
''Tunawataka wazazi kuboreha elimu ya watoto wao .Tunawakubusha watoto kuwa wanapaswa kuheshimu mamlaka,na kuwa umri wa kuwajibishwa ni miaka 15
Walikamatwa walipokuwa katika shule ya ECOFO iliyopo katika mkoa wa kaskazini wa Burundi wa Kirundo tarehe 12 mwezi Machi ,2019
Awali walishitakiwa wakiwa wanafunzi saba, lakini wanne wakaachiliwa huru.
Watatu hao walikua wanashikiliwa kwenye gereza la wanawake la mkoa wa Ngozi.
Mnamo mwaka 2016 shule mbali mbali mjini Bujumbura na mikoani watoto kadhaa walitiwa mbaroni wakihusishwa na matukio ya aina hiyo.
Shirika la kutetea watoto FENADEB lilikua msitari wa mbele kuwatetea watoto hao.
Mashirika ya kutetea haki za watoto nchini Burundi yameshauri uchunguzi wa kina ufanyikekabla ya kuwatia watoto hao hatiani ili kubaini ni kwa nini matukio kama hayo yanajitokeza.

Na Joseph Shaibu.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAFUNZI WALIOKAMATWA KWA KUMKEJELI RAIS PIERRE WAACHIWA HURU
Reviewed by By News Reporter
on
3/28/2019 08:44:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: