Loading...

BOEING 737 MAX YA SHIRIKA LA NDEGE LA SOUTHWEST AIRLINES YATUA KWA DHARULA

Loading...
Ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la Southwest, iliyokuwa ikisafiri kwenda California kuegeshwa kutokana na marufuku yanayozikabili ndege hizo na ambayo haikuwa na abiria, imelazimika kutua kwa dharura, shirika hilo limesema.

Katika taarifa yake, Southwest Airlines imesema kuwa ndege hiyo ilijulikana kuwa ina tatizo la kimitambo lisilo husiana na lile linalochunguzwa kama sababu ya ajali ya ndege mbili za aina hiyo ya Boeing 737 MAX, nchini Ethiopia mwanzoni mwa mwezi huu wa Machi na indonesia mwezi Oktoba mwaka jana.

"Wafanyakazi wa ndege hiyo walifuatilia maelekezo na kulazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orlando na wote wako salama. Ndege hiyo ililazimika kutua baada ya kuona kuwa inatatizo kwenye moja ya injini zake, shirikala ndege la Southwest Airlines limebaini.

Ndege hiyo ilitarajiwa kusafiri kwenda uwanja wa ndege wa Victorville, huko California, karibu na jangwa la Mojave, eneo ambako Southwest ilianza kutuma ndege zake aina ya MAX kwa minajili ya kuhufadhiwa.

Kampuni ya Boeing imealika marubani zaidi ya 200, viongozi na wasimamizi mbalimbali kuhudhuria kikao cha mafunzo kuhusu mpango wake wa unaolenga kuunga mkono uanzilishwaji upya wa safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX, ambapo kampuni hiyo ya Marekani itatoa maelezo kuhusu kupitia upya programu ya Boeing 737 MAX.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BOEING 737 MAX YA SHIRIKA LA NDEGE LA SOUTHWEST AIRLINES YATUA KWA DHARULA BOEING 737 MAX YA SHIRIKA LA NDEGE LA SOUTHWEST AIRLINES YATUA KWA DHARULA Reviewed by By News Reporter on 3/28/2019 08:26:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.