Loading...

DAKTARI WA KOREA ATEKWA NYARA NCHINI NIGERIA

Loading...
Daktari mmoja raia wa Korea Kaskazini atekwa nyara nchini Nigeria.

Msemaji wa jeshi la Polisi Muhammed Shehu amefahamisha kwamba daktari mmoja raia wa Korea Kaskazini kwa majina Jen Sunail alitekwa akiwa nyumbani kwake siku ya Jumatatu usiku.

Shehu alisema kwamba kutokana na daktari huyo kutokwenda kazini, madaktari wenzie walitoa taarifa polisi. Polisi walianzisha oparesheni maalumu kwa ajili ya kumtafuta daktari huyo.

Ingawa adhabu kwa wale wanaoteka watu kwa ajili ya kudai fidia katika majimbo mengi nchini Nijeria ni kifo, bado vitendo hivyo vya utekaji vimekuwa vikiendelea kutokea.
Na George Owino.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DAKTARI WA KOREA ATEKWA NYARA NCHINI NIGERIA DAKTARI WA KOREA ATEKWA NYARA NCHINI NIGERIA Reviewed by By News Reporter on 3/28/2019 08:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.