Loading...
Umoja wa ulaya umepitisha mswada wa sheria ambapo kuanzia mwaka 2022 na kuendelea magari mapya yote yatapaswa kuwa na mfumo wa kidhibiti mwendo.
Baraza la Umoja wa Ulaya limefahamisha kwamba muswada wa sheria ambayo inataka teknolojia mpya ya usalama kuwekwa kwenye magari umepitishwa.
kwa mujibu wa muswada huo kuanzia mwaka 2022 na kuendelea magari mapya madogo, malori na mabasi yatawekewa mfumo wa usalama utakaojumuisha kidhibiti mwendo otomatiki, mfumo wa breki wa dharura,mfumo wa kufuata njia, mfumo wa kugundua uchovu, mfumo wa kamera. Mifumo yote hiyo itakuwa ni ya matumizi ya lazima.
Pia katika kuruhisha uchunguzi wakati wa ajali zinapotekea magari yote yatawekwa mfumo wa boxi jeusi kwa ajili ya kurekodi taarifa za safari.
Ili mifumo hiyo ya teknolojia mpya ianze kutumika rasmi itabidi muswada huo wa sheria uidhinishwe kuwa sheria na bunge la Ulaya pamoja na baraza la Umoja wa Ulaya.

Na Francis James.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAGARI SASA KUWEKEWA VIDHIBITI MWENDO, MPANGO KUANZA ULAYA
Reviewed by By News Reporter
on
3/28/2019 07:54:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: