Loading...
WAKALA wa Chukula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imeteketeza samaki tani 106 walioingizwa nchini kutoka China na maziwa tani 23 kutoka Dubai baada ya kuonekana hayafai kwa matumizi ya binaadamu.
Samaki hao waliokuwa kwenye makontena manne ya futi 40 waliingizwa na kampuni ya Drive Shark na kontena moja la maziwa kutoka Dubai yaliletwa na mfanyabiashara Yunus Hashim.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuharibu bidhaa hizo jaa la Kibele, Ofisa Uhusiano wa ZFDA, Abdulmatin Yassin alisema samaki waliharibika baada ya kukosa umeme wa uhakika kwenye makontena.
Alisema samaki wanapoingizwa nchini huwa wameganda na hutakiwa waendelee kubakia katika barafu wakati wote lakini wakati makontena yakisubiri kupakuliwa palitokea kasoro na kusababisha samaki kuharibika.
Alisema kwa upande wa maziwa yaliharibika baada ya baadhi ya maboksi kupasuka wakati yakisafirishwa kutoka Dubai kwenda Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa athari zitokanazo na chakula , Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar, Aisha Suleiman alisema samaki wanaoingia ni salama kwa matumizi ya binadamu lakini umakini unahitajika wakati wa usafirishaji.
Mmoja wa Maofisa kutoka kampuni ya Drive Shark, aliishauri serikali kushirikiana na mfanyabiashara husika kuangalia matumizi mbadala ya bidhaa za aina hiyo, kwa sababu hazina sumu, badala ya kupoteza fedha nyingi kuziharibu.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ZAIDI YA TANI 100 ZA SAMAKI ZATEKETEZWA NA ZFDA
Reviewed by By News Reporter
on
3/28/2019 07:45:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: