Loading...

JAMAA AJIKATA MGUU WAKE MWENYEWE BILA GANZI KISA GHARAMA ZA MATIBABU

Loading...
Jamaa mmoja kutoka Ukraine aliwafanya maafisa wa polisi waanzishe uchunguzi kuhusu madai ya mauaji baada yake kuukata mguu wake wa kulia akitumia kisu. 

Vladimir Tverdokhleb alihoji kuwa mguu wake huo ulikuwa umeathirika kiasi cha kuoza, hivyo basi suluhu aliokuwa nalo kwa wakti huo ni kuukata.

Kulingana na shirika la Daily Mail, mzee huyo mwenye umri wa miaka 62, alitekeleza kitendo hicho machoni pa mkewe aliyesimulia kuwa hamna dawa yoyote aliyomeza kabla na baada ya kuukata mguu huo. 

Vladimir baadaye aliutupa mguu huo kwenye jaa la taka ambapo mbwa wa jirani yake aliuokota.

Mbwa huyo aliubeba mguu huo hadi kwao lakini kabla ya kuukalia na kuufanya kitoweo, mkaazi mmoja aliuona na kusongea karibu kutaka kupeleleza zaidi kuhusu kile alichokuwa amekiona. 

Baada ya uchunguzi wa karibu, mkaazi huyo aliyejulikana kama Irina, aligundua kuwa ulikuwa ni nyama ya binadamu wakati aliona vidole na makucha.

"Mwanzoni, sikuweza kubaini kilichokuwa kimebebwa na mbwa huyo, lakini wakati nilipeleleza zaidi niliona vidole vya mguu na makucha. Nilihisi kuchanganyikiwa," Irina alisimulia. 

Papo hapo, aliwapigia maafisa wa polisi waliofika na kuanzisha uchunguzi baada ya kubaini kuwa ulikuwa ni mguu wa binadamu waliyeshuku alikuwa ameuawa.

Hata hivyo, uchunguzi huo ulisitishwa ghafla baada ya maafisa hao kugundua kuwa mguu huo uliooza ulikuwa wa Vladimir. 

Vladimir alikimbizwa hospitalini kufuatia tukio hilo ili kupata matibabu zaidi. 

Alipoulizwa ni kwa nini aliamua kutekeleza kitendo hicho, alihoji kuwa hakuwa na fedha za kulipa hospitalini ndiposa mguu huo ukatwe.
Na Mary Mkeu.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JAMAA AJIKATA MGUU WAKE MWENYEWE BILA GANZI KISA GHARAMA ZA MATIBABU JAMAA AJIKATA MGUU WAKE MWENYEWE BILA GANZI KISA GHARAMA ZA MATIBABU Reviewed by By News Reporter on 3/27/2019 08:15:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.