Loading...
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewasimamisha kazi maafisa watatu wa ikulu baada ya zaidi ya nguruwe 900 kutoweka wasijulikane waliko
Kulingana na taarifa tulizozipokea hapa Dundiika News, Nguruwe hao walikuwa wapelekewe wakazi wa Kityerera wilaya ya Mayuge ili wakafugwe. Maafisa hao walilaumiwa kwa kushindwa kuelezea walikokwenda nguruwe hao huku taarifa za kuaminika zikiarifu kuwa huenda waliuzwa kisiri.
Kulingana na taarifa za jarida la Daily Monitor, maafisa hao watatu akiwemo Moses Basoga, Sarah Kawuma na Waitah Atim walipatiwa likizo ya lazima huku uchunguzi ukianzishwa kubaini ni vipi nguruwe hao walivyotoweka.
Imesemekana Rais Museveni aliwaahadi wakazi wa Kityerera wakati wa kampeni kwamba angewapatia nguruwe hao ili waboreshe maisha yao kupitia ufugaji.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NGURUWE 945 WA RAIS MUSEVENI WAIBIWA, MAAFISA WA IKULU MATATANI
Reviewed by By News Reporter
on
3/27/2019 08:04:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: