Loading...

KENYA: MTANGAZAJI MANUSURA AJIFUNGUE AKIWA ANASOMA TAARIFA YA HABARI

Loading...
Mtangazaji aliyekuwa mjamzito wa kituo cha KTN cha nchini Kenya, bi Czeda Brenda alishikwa na uchungu wa mimba alipokuwa akirusha matangazo kwenye makala ya Easy Friday.

Muziki ulichezwa kwa sekunde chache kabla ya mtangazaji mwenzake, Stevens Mueno kuchukua nafasi yake huku Brenda akikimbizwa katika hospitali ya Nairobi kwenye ambulansi. 

Licha ya kuwa mjamzito, mtangazaji huyo amekuwa akisimamia makala hayo ya Easy Friday hadi dakika za mwisho.

Brenda alijiunga na shirika la utangazaji la The Standard mwaka wa 2018 baada ya kufanya kazi kwa miaka kadhaa katika shirika la utangazaji la KBC. Dundiika News inamtakia mtangazaji huyo kila la kheri anapomkaribisha mtoto wake kipenzi duniani.
Na Ummy Zuberi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KENYA: MTANGAZAJI MANUSURA AJIFUNGUE AKIWA ANASOMA TAARIFA YA HABARI KENYA: MTANGAZAJI MANUSURA AJIFUNGUE AKIWA ANASOMA TAARIFA YA HABARI Reviewed by By News Reporter on 3/30/2019 07:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.