Loading...

TAFITI: MABADILIKO HALI YA HEWA YASABABISHA KUONGEZEKA KWA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA

Loading...
Utafiti uliofanywa umeonyesha kwamba mabadiliko ya hali ya hewa na kuongezeka kwa joto duniani kutasababisha magonjwa ya kuambukiza kwa mbu kuongezeka zaidi.

Wanasayansi wameonya kwamba mpaka kufikia mwaka 2080 watu zaidi ya bilioni 1 wanaweza kuwa wameathiriwa na magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya mbu. Hilo linatokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongezeka kwa joto.

Kwa mujibu wa matokeao ya utafiti yaliyotolewa na maktaba ya jamii ya sayansi nchini Marekani, Kuongezeka kwa joto duniani kunasababisha magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya mbu kama vile Zika, Chikungunya, na homa ya Denge kuenea kwa urahisi zaidi.

Utafiti huo umeonyesha kwamba magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya mbu yameongezeka. Utafiti huo pia unatazamia magonjwa hayo yataongezeka zaidi hasa katika nchi za Marekani, Amerika ya kati, Asia ya mashariki ,Afrika ya mashariki na Kanada.

Katika utafiti huo kufikia mwaka 2050 karibu watu nusu bilioni, na kufikia mwaka 2080 zaidi ya watu bilioni 1 watakuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa yanayoenezwa na mbu.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani kila mwaka watu zaidi ya milioni hupoteza maisha kutokana na malaria na magonjwa mengine yanayofanana na malaria.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAFITI: MABADILIKO HALI YA HEWA YASABABISHA KUONGEZEKA KWA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA TAFITI: MABADILIKO HALI YA HEWA YASABABISHA KUONGEZEKA KWA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA Reviewed by By News Reporter on 3/30/2019 07:53:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.