Loading...

MGODI WAPOROMOKA, 14 WAPOTEZA MAISHA NCHINI DRC

Loading...
Watu 14 wamepoteza maisha baada ya mgodi wa madini ya Koltan kuporomoka  mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa habari kutoka vyanzo vya ndani vya nchi hio, Mvua kubwa zilizonyesha nchini humo zimepelekea mgodi wa madini ya Koltani unaopatika katika eneo la Niyabiwe kuporomoka.

Mmoja wa viongozi wa eneo hilo Muhima Kateete, alisema miili ya watu 14 waliopoteza maisha ilipatikana baada kufukua mgodi huo. Watu wengine 9 waliokolewa wakiwa wamejeruhiwa.

Ajali za kuporomoka kwa migodi hutokea mara kwa mara nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na usalama mdogo katika migodi hiyo.
Na Vicky Frank.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MGODI WAPOROMOKA, 14 WAPOTEZA MAISHA NCHINI DRC MGODI WAPOROMOKA, 14 WAPOTEZA MAISHA NCHINI DRC Reviewed by By News Reporter on 3/30/2019 08:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.