Loading...
Uganda. Ajuza mwenye umri wa miaka 80 amezua gumzo baada ya kusema umri si kitu na kurejea shuleni kuanza kusoma na wajukuu zake.
Maria Obonyo aliwashangaza na kuwafanya wanafunzi kuchangamka sana baadaya kuamua kusoma nao licha ya umri wake mkubwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, ndoto ya ajuza huyo ni kuwa mwalimu mara pindi akihitimu masomo yake.
Akihojiwa na wanahabari, Maria alisema aliamua kurejea shuleni baada ya ndugu na jamaa zake kuaga dunia na hamna mtu wa kumwangalia uzeeni.
"Hamna mtu wa kuniangalia. Jamaa zangu wote waliaga dunia na ndio maana nikaamua kuja shuleni. Ninaamini nitatia bidii hadi Chuo Kikuu cha Makerere na nikifuzu niwe mwalimu," Maria alisema.
Ajuza huyo alisema kuwa, mara akimaliza masomo yasekondari atajiunga na chuo kikuu ili waliokuwa wakimcheka hajui kusoma wala kuandika wapate aibu.
Kulingana na Stella Tayona, mkurugenzi wa shule anakosomea Maria, mwanafunzi huyo alijiunga na shule hiyo kutokea chekechea ya chini na kuibuka wa kwanza.
"Ni mwanafunzi mwenye bidii sana, hakosi kuhudhuria masomo na ni rafiki wa kila mtu," Tayona alisema.

Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KIKONGWE WA MIAKA 80 NA NDOTO ZA UALIMU, ARUDI SHULE
Reviewed by By News Reporter
on
3/08/2019 10:08:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: