Loading...

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: WANAWAKE WA ETHIOPIA KURUSHA NDEGE BILA WANAUME

Loading...
Shirika la Ndege la Ethiopia wanasherehekea siku ya mwanamke duniani kwa wanawake pekee kuendesha ndege na kufanya shughuli zote za kiofisi pasipo wanaume. Na watafanya safari kuanzia Addis Ababa to Oslo.

Shirika hilo lilitangaza rasmi taarifa hiyo kupitia mtandao wa Twitter na Facebook kwamba: "Wanaweke siku ya Machi 8, ndio watakao tawala anga na ardhi kuhakikisha ndege zinafanya safari zake kama kawaida ila kuonyesha kuwa wanawake wanaweza."

Hii inamaanisha warusha ndege, waongozaji wa ndege, walinzi, wahudumu wa chakula, makuli, watu wa usafi, trafiki wa anga wote watakuwa wanawake kwa siku ya leo.

Nchi nyingine ambazo zilishawahi kufanya kama Ethiopia ni India, mwaka jana ambapo karibia ndege zote zilizoruka kutoka India kwenda katika mataifa mengine ziliendeshwa na wanawake.

Mwaka jana, pia Uingereza ilifanya kitu kama hicho, ambapo wanawake walirusha moja ya ndege kubwa ikitokea London Heathrow hadi Glasgow - ambayo ilihusisha jumla ya wanawake 60.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: WANAWAKE WA ETHIOPIA KURUSHA NDEGE BILA WANAUME SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: WANAWAKE WA ETHIOPIA KURUSHA NDEGE BILA WANAUME Reviewed by By News Reporter on 3/08/2019 09:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.