Loading...

RAIS KAGAME ADHURU TANZANIA, KUYAJENGA NA JPM

Loading...
Rais wa Rwanda, Paul Kagame ametua Tanzania jana Alhamisi, Machi 7, 2019 kwa ziara ya siku mbili ambapo atafanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Katika uwanja wa ndege wa zamani (Terminal 1), Rais Kagame amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi.

Pia, kulikuwapo na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu aa Wilaya ya Kinondoni, Daniel  Chongolo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri.

Baada ya kupokelewa, Rais Kagame na msafara wake wameelekea Ikulu ya Dar es Salaam.
Rais Kagame amekuja Tanzania wakati uhusiano wake na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ukilegalega huku mpaka kati ya Rwanda na Uganda ukifungwa.

Rwanda imesema mpaka huo wa Gatuna umefungwa kwa sababu ya ujenzi wa barabara unaoendelea.

Wakati Rais Kagame akipokea uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) nchi yake imeingia kwenye mzozo mwingine na nchi ya Burundi.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS KAGAME ADHURU TANZANIA, KUYAJENGA NA JPM RAIS KAGAME ADHURU TANZANIA, KUYAJENGA NA JPM Reviewed by By News Reporter on 3/08/2019 08:30:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.