Loading...
Idara ya masuala ya anga na Urubani ya Marekani (NASA) imetangaza itatoa mshahara wa dola za kimarekani 18,500 ( Karibu Mil. 43 za kiTanzania) kwa watu watakaojitolea kushiriki utafiti wao utakaodumu kwa miezi 2.
Watu hao watakaojitolea watahitajika kulala katika chumba maalum bila kufanya kazi nyingine yeyote.
Nasa inatarajia kufanya utafiti kuhusu madhara ya kani ya mvutano katika afya. Idara hiyo inatafuta watu 24.
Kwa ajili ya Utafiti huo watahitajika watu wenye umri kati ya miaka 24 na 55, Kati ya watakaomba watachaguliwa wanawake na wanaume12.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BBC, NASA kwa kushirikiana na Idara ya anga ya Ulaya wataendesha utafiti huo nchini Ujerumani katika kituo cha anga cha Kolon.
Utafiti huo unatarajiwa kuanza mwezi Septemba. Maombi yatapokelewa mpaka Mei 24. Waombaji wanapaswa kufahamu lugha ya Kijerumani.
Wataalamu wa NASA wameshauri waombaji hao ni vizuri wakawa na hobi ya kusoma vitabu na kuangalia Tv, ili kuwasaidia wasichoke watakapokuwa kwenye chumba hicho.
Watakaochaguliwa kushiriki katika utafiti huo watakuwa na muda kwa ajili ya kujizoesha mazingira ukijumuisha na muda wa utafiti kwa ujumla watakuwa katika kituo hicho cha anga kwa muda wa siku 89.

Na Mary Mkeu.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NASA YATANGAZA KAZI YA KULALA KWA MSHAHARA WA ZAIDI MIL. 43/-
Reviewed by By News Reporter
on
3/29/2019 06:54:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: