Loading...

TANGAZO KWA UMMA: ONYO KWA MAFUNDI WA KUWEKA MIFUMO YA UMEME

Loading...
Taarifa inatolewa kwa mafundi wa umeme na umma kwa ujumla kuwa:- 

(a)  Ni kosa kisheria kufanya kazi za kuweka mifumo ya umeme (electrical installation) bila kuwa na leseni hai iliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Hivyo basi, ili kukidhi matakwa ya sheria ya Umeme, kila fundi umeme anayefanya kazi za kuweka mifumo ya umeme, lazima awe na leseni iliyo hai iliyotolewa na EWURA.

(b)  EWURA inatoa tahadhari kwa mafundi umeme wanaotoa huduma za uwekaji wa mifumo ya umeme bila kuwa na leseni halali kuacha mara moja na kuomba leseni EWURA.

(c)  Mafundi wote ambao hawana leseni wanaweza kuomba kutumia mfumo wa kieletroniki wa Licensing and Ordering Information System (LOIS) uliopo kwenye Tovuti ya EWURA "www.ewura.go.tz" au kwa kufika makao makuu ya EWURA, Dodoma au ofisi za Kanda za Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha.

(d)  EWURA itafanya ukaguzi endelevu kuwabaini wote watakaoendelea kutoa huduma za uwekaji wa mifumo ya umeme bila ya kuwa na leseni, hivyo basi, watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Ili kurahisisha utambuzi, wale wote wenye leseni wanatakiwa kuwa na leseni kila wawapo kazini na wazioneshe pale watakapotakiwa kufanya hivyo na wakaguzi au na wateja wao.

(e)  Wateja wa huduma za uwekaji mifumo ya umeme wanaaswa kuepuka kutumia mafundi wasiokuwa na leseni. Kwa utambuzi ni vyema kuomba kitambulisho cha fundi husika au kutumia orodha ya mafundi inayopatikana kwenye tovuti ya EWURA (www.ewura.go.tz).
Na John Mbiki.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TANGAZO KWA UMMA: ONYO KWA MAFUNDI WA KUWEKA MIFUMO YA UMEME TANGAZO KWA UMMA: ONYO KWA MAFUNDI WA KUWEKA MIFUMO YA UMEME Reviewed by By News Reporter on 3/23/2019 09:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.