Loading...

UGANDA: RAPA WA MIAKA 7 AZUILIWA KUFANYA MUZIKI KISA MWANAFUNZI

Loading...
Serikali ya Uganda imemuamurisha mvulana wa miaka 7 ambaye pia ni rapa chipukizi kuachana na mambo ya muziki na badala yake arudi shuleni na afanye bidii masomoni.

Waziri wa mambo ya vijana na watoto Florence Nakiwala alionya kwamba Patrick Ssenyonjo ama kwa majina ya usanii Fresh Kid atakamatwa iwapo atapatikana akifanya onyesho lolote la muziki. 

Akizungumza kwenye mahojiano na NBS TV, waziri huyo alisema kulingana na sheria ya kazi nchini humo, mvulana huyo hajahitimu umri wa miaka 18 unaomruhusu kufanya kazi.

Nakiwala alidai mvulana huyo atashindwa kwenda shuleni kila siku kwa ajili ya kujishughulisha sana na muziki huku rika lake ni la kwenda shule. 

Waziri huyo alionya kuwa atamchukulia hatua kali za kisheria rapa huyo pamoja na meneja wake endapo atapatikana akifanya muziki. 

Hata hivyo, meneja wake alimtetea Fresh Kid akisema yeye hufanya onyesho wikendi tu na tangu mwaka huu uanze ametumbuiza katika matamasha mawili pekee.
Na Frank Malogo.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UGANDA: RAPA WA MIAKA 7 AZUILIWA KUFANYA MUZIKI KISA MWANAFUNZI UGANDA: RAPA WA MIAKA 7  AZUILIWA KUFANYA MUZIKI KISA MWANAFUNZI Reviewed by By News Reporter on 3/29/2019 08:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.