Loading...

WANAFUNZI 7 MBARONI KWA KUMKOSEA HESHIMA RAIS NKURUNZINZA

Loading...
Ingawaje mataifa ya Kiafrika yamepiga hatua katika kuzingatia uhuru na haki za kibinadamu, nchi ya Burundi imesalia nyuma katika kuafiki uhuru wa kujieleza. 

Haya yanadhihirika wazi kufuatia misimamo mikali yake rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza, kwa yeyote anayejaribu kuipa serikali yake changamoto na kumpinga katika mtindo wake wa uongozi.

Kulingana na ripoti za shirika la haki za kibinadamu- Human Rights Watch, hivi maajuzi maafisa wa polisi wamewakamata watoto saba wa shule kwa ajili ya kuchora picha ya rais huyo kwenye vitabu vyao. 

Baada ya kupelekwa kwa mwendesha mashtaka ya umma ya nchini humo katika eneo la Kirundo, mmoja wao aliyekuwa na miaka kumi na tatu aliachiliwa huru kwa kuwa umri wake ulikuwa mdogo.

Sita kati yao walizuiliwa katika kituo cha polisi na baadaye watatu wakaachiliwa huru na kuruhusiwa kuenda nyumbani. 

Waliosalia mbaroni walifunguliwa mashtaka ya kumkosea heshima rais wa nchi hiyo, na iwapo watapatwa na hatia basi watafungwa jela kwa miaka tano. 

Aidha, hii sio mara ya kwanza kwa serikali kuendesha oparesheni katika utawala wa shule nchini humo kuwasaka wanaomkosea heshima rais. 

Mwaka wa 2016, wanafunzi wanane walikamatwa na idara ya upelelezi kwa hatia ya kuchora picha yake Nkurunziza kwenye vitabu vyao na kunakili jumbe za, "Ondoka" na "hamna muhula wa tatu." 

Mwaka huo huo wanafunzi wengine walifukuzwa shuleni kwa kuchora uso wake rais katika vitabu vyao pia.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAFUNZI 7 MBARONI KWA KUMKOSEA HESHIMA RAIS NKURUNZINZA WANAFUNZI 7 MBARONI KWA KUMKOSEA HESHIMA RAIS NKURUNZINZA Reviewed by By News Reporter on 3/22/2019 08:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.