Loading...
Mwanamke mmoja mwenye umri wa makamo kutoka Afrika Kusini amegusa nyoyo za maelfu ya wananchi kwa kujitolea kuwasaidia watoto zaidi ya 400 wanaotoka katika familia zisizojiweza.
Waswahili wanasema kidogo kula mwenzako, hasa yule mwenye uhitaji. Mwanamke huyu shupavu aliliona mapema ndipo akaamua kujitosa mzima mzima kuwagawia kidogo majirani zake alichobarikiwa mwenyezi Mungu.
Shanaaz Allie alizindua mradi maalum wa 'Mosadie' ambao anaundesha kutumia fedha zake bila ya kupata misaada kutoka kwa mashirika yoyote.
Mfanyabiashara huyo amejitolea kuwaandalia chakula watoto 400 kila mwezi na huhakikisha kwamba anawapatia lishe bora zaidi.
Kulingana na taarifa tulizozipokea hapa Dundiika News Allie hutumia takriban Sh. milioni 1.2 kugharamia chakula cha watoto hao ambao wengi ni wa majirani wake.
"Huwa naandaa chakula kitamu sana, nilikuja hapa kumsaidia kupika vyakula kadhaa na nilimpata akiwa ashapika biriani na kwa kweli ilikuwa ya kudondosha mate," Mmoja wa marafiki wake alisema.
Allie alilelewa na familia isiyojiweza na anayaelewa vizuri maisha magumu ndio sababu amejitolea kurudisha mkono kwa jamii.
Na Catherine Kisese.

.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KUTANA NA MWANAMKE ANAYELISHA WATOTO 400 WA MAJIRANI KWA PESA YAKE BINAFASI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
4/03/2019 10:14:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: