Loading...

MAANDAMANO YAZIDI KUTIKISA SUDAN HUKU KIONGOZI WA BARAZA LA MPITO ATANGAZA KUJIUZULU

Loading...
Waziri wa ulinzi aliyeapishwa Alhamisi, Aprili 11 kuwa rais wa baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan Ahmed Awadh Auf amejiuzulu. 

Awadh Auf alitangaza kujiuzulu Ijumaa, Aprili 12, siku moja baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani rais Omar al-Bashir na yeye kuchukua hatamu. Sasa nafasi hiyo imetwaliwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan Abdulrahman, BBC imeripoti.

Wakati akitoa taarifa ya kujiuzulu kupitia televisheni, Awadh Auf alisema anaachia wadhifa huo kwa maslahi ya taifa na kwa kuwa taifa hilo lina watu wazuri na jeshi la kuaminika. Alisema ana imani kubwa makundi hayo mawili yatafanya kazi pamoja. 

Dundiika News inafahamu kuwa, Auf ambaye anakabiliwa na vikwazo kutokana na ushiriki wake kwenye mauaji ya wakati wa mgogoro Darfur alikuwa akifuatwa na shinikizo kutoka kwa waandamanaji na kimataifa akitakiwa kuanzisha serikali ya mpito ya kiraia licha ya jeshi kuwahakikishia raia halingekaa uongozini muda mrefu.

Licha ya kuondoka kwa al Bashir, waandamanaji wamekuwa wakiendelea kuandamana wakisema hawakufurahishwa kuona nafasi yake inachukuliwa na waziri wa ulinzi ambaye wanadai ni sehemu ya serikali ya rais huyo ambaye alikuwa madarakani kwa miongo mitatu. 

Kufuatia hali nchini humo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa ndani Ijumaa, Aprili 12, kufuatia ombi la Marekani, Ubelgiji, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Poland.

Katika ripoti ambayo Dundiika News imeisoma, Balozi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa Christoph Hausgen aliwaambia wanahabari baada ya mkutano kwamba kunatakiwa kuwepo na mpango wa kisiasa wenye haki na jumuishi.

Kulingana naye, al-Bashir anatakiwa kwenda Mahakama ya Kimataifa kuhusu Jinai (ICC) ya The Hague na mataifa yanajukumu la kumkabidhi katika mahakama hiyo. 

Mkutano mwingine wa baraza hilo utafanyika Jumatatu, Aprili 15, kujadiliana kuhusu hali itakavyokuwa nchini humo.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAANDAMANO YAZIDI KUTIKISA SUDAN HUKU KIONGOZI WA BARAZA LA MPITO ATANGAZA KUJIUZULU MAANDAMANO YAZIDI KUTIKISA SUDAN HUKU KIONGOZI WA BARAZA LA MPITO ATANGAZA KUJIUZULU Reviewed by By News Reporter on 4/14/2019 08:31:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.