Loading...

JAMAA ANASWA 'LIVE' AKIMLA URODA MBUZI, MAJIRANI WAMSHUSHIA KICHAPO

Loading...
Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 45 huko Kakamega, Kenya anauguza majeraha mabaya baada ya kupokezwa kichapo cha mbwa na wenyeji waliojawa na hamaki baada ya kufumania peupe akishiriki ngonona mbuzi wa jirani.

Kwa mujibu wa jarida la TUKO la nchini Kenya ni kwamba, jamaa huyo kwa jina Justus Mbakaya, almaarufu Jokinda kutoka kijiji cha Rostaman eneo bunge la Lurambi Kaunti ya Kakamega alipatikana akifanya kitendo hicho usiku wa Jumatan, Aprili 10, baada ya jirani kumsikia mbuzi wake akitoa sauti zisizokuwa za kawaida. 

Alipokwenda kuangalia kilichokuwa kikiendelea, alipigwa na butwaa kubwa alipomuona mwanamume juu ya mbuzi wake.

Akizungumza na TUKO mke wa mshukiwa Elizabeth Inziani alisema kuwa, maisha yao ya ndoa yamekuwa na taabu nyingi na mume wake amekuwa akimtimua kila mara. 

Kulingana naye, mume wake amekuwa akimtunza mbuzi huyo kama kitu cha thamani sana na tabia hiyo imekuwa ikimshangaza hadi mumewe pale alipofumaniwa akifanya kitendo hicho. 

"Kwa muda mrefu tumekuwa tukijiuliza mbona mume wangu amekuwa akimpenda sana mbuzi huyu. Mara nyingine utapata anampeleka malishoni bila kuambiwa na mtu yeyote ikizingatiwa kuwa mbuzi huyo si wetu.

"Na ikifika jioni anapenda kumfunga karibu na boma letu, leo ndio tumejuwa ukweli wa mambo amepatikana juu ya mbuzi na tunaushuku ujauzito ambao mbuzi huyo anao ni wake," Inziani alisema.

Zaidi ya kufanya mapenzi na mbuzi wa jirani, inadaiwa Jokinda amekuwa akimbaka mwanawe mwenye umri wa miaka 15 ambaye akili zake si timamu na hata amepachika mimba.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JAMAA ANASWA 'LIVE' AKIMLA URODA MBUZI, MAJIRANI WAMSHUSHIA KICHAPO JAMAA ANASWA 'LIVE' AKIMLA URODA MBUZI, MAJIRANI WAMSHUSHIA KICHAPO Reviewed by By News Reporter on 4/14/2019 08:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.