Loading...

MOMBASA: MAHARUSI WABADILISHA ENEO LA HARUSI KISA WAPENZI WAO WA ZAMANI

Loading...
Kulizuka purukushani katika kanisa la Global Apostolic Missions mjini Mombasa, baada ya mke wa zamani wa bwana harusi na mume wa zamani wa bi harusi kuwasili wakitaka sherehe ya harusi ya wapenzi wao wa zamani kusitishwa mara moja. 

Inakisiwa kuwa, awali maharusi hawa walilazimika kubadilisha eneo la hafla yao na kuiandaa kanisani ili kuwakwepa wachumba wao wa zamani lakini mpango wao ulionekana kutozaa matunda.

Kulingana na ripoti ya KTN News, washiriki wa kanisa hilo walilazimika kuifunga milango wakati wa sherehe hiyo, wakisema kuwa fursa ya kuhudhuria ilipewa watu wachache pekee.

Wachumba hao wazamani hawakuwa na buda ila kuchungulia dirishani maharusi wakivishana pete. 

"Tulioana mwaka wa 2005 na tukabarikiwa na watoto watatu kwa muda wa miaka 12....Kile ninadai ni harusi ii isitishwe mara moja ndiposa tushauriane na mme wangu jinsi watoto hao watasoma, sababu pekee yangu siwezi," Sheilla Robina ambaye ni mke wa zamani wa bwana harusi alisema. 

Wanaharakati wa haki za binadamu na polisi walioitwa ili kutuliza hali walikosa la kufanya kwani Robina alikuwa na vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao watatu wala sio cheti cha harusi kwani yeye na mumewe walifunga tu ndo ya jadi. 

Maafisa wa polisi walimshauri kutmbelea idara ya kutetea haki za watoto ndiposa apate usaidizi na mumewe ajukumike kuwalea wanawe. 

Mume wa zamani wa bi harusi naye alikuwa ametulia baada ya kushikwa na mshtuko wa kushuhudia mkewe na mama wa watoto wake akiozwa kwa bwana mwingine.
Na Bernard Felix.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MOMBASA: MAHARUSI WABADILISHA ENEO LA HARUSI KISA WAPENZI WAO WA ZAMANI MOMBASA: MAHARUSI WABADILISHA ENEO LA HARUSI KISA WAPENZI WAO WA ZAMANI Reviewed by By News Reporter on 4/14/2019 09:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.