Loading...

RAIS TRUMP: NIMEKWISHA, HUU NDIO MWISHO WA UTAWALA WANGU

Loading...
Imefahamika kwamba baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump,  kufahamu kwamba wakili maalum Robert Mueller ameteuliwa katika shauri la kuchunguza Urusi ilivyoshawishi ushindi wake wa uraisi mnamo mwezi Mei, 2017 alisema kwamba huo ndio ungekuwa mwisho wa urais wake.

Baada ya Raıs Trump kufahamu kwamba Muller  ameteulıwa kama wakili maaulum katıka shauri hilo alionyesha kutishika sana.

Ripoti yenye kurasa 400  juu ya shauri hilo imewekwa katika ukurasa wa mtandao wa wizara ya haki na sheria ya nchi hio.

Imeandikwa kwenye ripoti hiyo kwamba mwezi Mei 2017 Rais Trump alivyofahamu Kuteluliwa kwa Mueller kama mmoja wa mawakili wa shauri hilo alisema maneno yafuatayo;

“ Eeh Mungu, Hii ni mbaya sana. Huu ndio utakuwa mwisho wa utawala wangu. Kila mtu ananiambia kama huyu ni mmoja wa mawakili wa shauri hili ataniaribia uongozi wangu, Kwamba shauri hili litachukuwa muda mrefu na sitakuwa nauwezo wakufanya chochote, Hiki ni kitu kibaya kunitokea "

Ripoti hiyo inasema alikuwa akimlaumu sana waziri wa haki na sheria wa kipindi hicho, Jeff Session akihoji “ Jeff, imekuwaje umeruhusu hili litokee? Kwani kazi yako sio kunilinda ?”

Kwa upande mwingine  Ripoti hiyo imearifu kwamba mara kadhaa Trump alijaribu kuzuia shauri hilo lisiendelee, Kitu ambacho hakikubaliwa na maafisa waliokuwa wakihusika, wakikataa kushiriki katika kuzuia haki isitendeke.

Katika ripoti hiyo pia imearifiwa kwamba Trump alimuamuru aliyekuwa  mshauri wa sheria wa Ikulu ya Marekani kipindi fulani Don McGahn  Amfukute kazi Mueller, McGahn hakukubaliana na suala hilo jambo lililopelekea ajiuzulu nafasi yake.

William Barr, waziri wa haki na sheria wa Marekani alitoa taarifa hapo jana kwamba Mueller katika uchunguzi wake hakupata dalili yeyote inayoonyesha kwamba rais Trump au timu yake ya kampeni ilikuwa na ushirikiano wa siri na Urusi, uliowawezesha kushinda uchaguzi.
Na John Richard.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS TRUMP: NIMEKWISHA, HUU NDIO MWISHO WA UTAWALA WANGU RAIS TRUMP: NIMEKWISHA, HUU NDIO MWISHO WA UTAWALA WANGU Reviewed by By News Reporter on 4/20/2019 08:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.