Loading...

BURUNDI YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA NYUMBA ZA IBADA

Loading...
Wizara ya mambo ya ndani nchini Burundi yapiga marufuku kufunguliwa kwa nyumba za ibada mjini Bujumbura

Tangazo lililotolewa na wizara ya mambo ya ndani nchini Burundi limefahamisha kuwa ni marufuku mjini Bujumbura kufunguliwa kwa nyumba ya ibada bila  ya  mamlaka husika kupewa taarifa na  kuruhusiwa na serikali.

Katika miaka ya hivi karibuni, makanisa ya uamsho mjini Bujumbura yameongezeka kwa kiasi kikubwa huku yakiwa hayatambuliki  katika uongozi mkuu wa kanisa.

Idadi ya wakazi wa jiji la Bujumbura imeripotiwa kuzidi kuongeza kila mwaka na kufikia watu milioni 2.

Nchini Burundi, asilimia 80 ya raia wake ni wakristo huku  asilimia 10 ikiwa ni  waislamu na imani nyingine.

Viongozi wa  dini hawajatoa tamko lolote kufaatia sheria hiyo.
Na Zakaria Bernard.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BURUNDI YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA NYUMBA ZA IBADA BURUNDI YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA NYUMBA ZA IBADA Reviewed by By News Reporter on 4/20/2019 08:19:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.