Loading...

MAJOKA YALIVYOMFUKUZA IKULU RAIS WEAH WA NCHINI LIBERIA

Loading...
Kulizuka taharuki afisini mwa Rais wa Liberia George Weah Jumatano, Aprili 17, baada ya majoka mawili kuonekana ofisini kwake Ikulu. 

Mpaka imemlazimu rais huyo kuwahudumia wananchi wake akiwa nyumbani huku wafanyikazi wengine wanaohudumu katika jengo hilo wakitahadharishwa dhidi ya kukaribia mahali hapo.

Kwa mujibu wa Katibu wa kitengo cha Habari za Rais Smith Toby, majoka hayo walipatikana katika afisi za wizara ya mambo ya kigeni, eneo ambalo afisi ya rais huyo ipo, BBC iliripoti.

"Jengo la Wizara ya mambo ya nje lina pia ofisi ya rais, kwa hivyo walitoa taarifa ya kuwashauri wafanyikazi wa afisi hizo mbili kubakia nyumbani hadi kitendawili hicho kitakapoteguliwa," 

Hata hivyo, majoka hayo hawakuuawa kwani walijipenyeza na kurudi katika makazi yao kabla hatua yoyote kuchukuliwa. 

"Majoka hayo hawakuuawa...kuna shimo dogo katika jengo hilo ambalo wawili hao walipitia na kurudi katika makao yao," Toby alisema. 

Tobby alifichua kuwa, huenda majoka hayo waliweka makaazi katika afisi hiyo kutokana na mazingira mabovu ya jengo hilo ambalo alisema lilijengwa miaka mingi. 

Kutokana na kisa hicho, hali ya usalama umeimarishwa katika makazi ya rais huyo huku magari ya msafara wake yakisalia kuegeshwa nje ya nyumba yake eneo la Monrovia, mji mkuu wa nchi hiyo.
Na Zahoro Bakari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAJOKA YALIVYOMFUKUZA IKULU RAIS WEAH WA NCHINI LIBERIA MAJOKA YALIVYOMFUKUZA IKULU RAIS WEAH WA NCHINI LIBERIA Reviewed by By News Reporter on 4/20/2019 08:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.