Loading...

13 WAFARIKI KWA KUPOROMEKEWA NA KANISA KATIKA IBADA YA IJUMAA KUU

Loading...
Waumini waliokuwa wamekusanyika kuadhimisha Ijumaa Kuu walikumbwa na mkasa baada ya jumba walimokuwa kuporomoka na kuwaua watu 13 huku wengine wengi wakinusurika lakini kwa majeraha mbalimbali. 

Kanisa hilo la Pentekote la Dlangubo, KwaZulu-Natal, Afrika Kusini lilikuwa limejaa waumini waliokuwa wakishiriki maandamano ya Ijumaa Kuu wakati upepo mkali na kimbunga vilipotokea na kusababisha jumba hilo kuporomoka Ijumaa, Aprili 19.

Lennox Mabaso, msemaji wa mamlaka ya eneo hilo, alithibitisha kutokea kwa mkasa huo na kuongezea kuwa, jumla ya watu 29 walipelekwa hospitalini. 

"Jumba lililokuwa likitumiwa na waumini wa Kanisa la Pentekote liliporomoka na kuwaua watu wanaokisiwa kuwa 13," alisema.

Maafisa kutoka Kituo cha Kukabilianana Mikasa walikuwa wakitarajiwa kumpeleka afisa mkuu wa uongozi eneo hilo Nomusa Dube-Ncube, ili kuona ni vipi familia zilizoathirika zitakavyosaidiwa. 

Dundiika News imeng’amua kuwa, maeneo ya Pwani ya Kaskazini yalikumbwa na kimbunga huku makundi ya uokoaji yakisema hali ilikuwa ngumu sana usiku.

Inadaiwa kuwa, majumba manne yaliporomoka, ajali tisa za magari na maeneo mengi kukumbwa na mafuriko viliripotiwa.

“Wakaazi walikosa umeme, nyumba na vitu vingine vilifurika maji na mali nyingi zilipeperushwa na upepo” shirika moja la uokoaji lilisema.
Na Saidi Jumbe.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
13 WAFARIKI KWA KUPOROMEKEWA NA KANISA KATIKA IBADA YA IJUMAA KUU 13 WAFARIKI KWA KUPOROMEKEWA NA KANISA KATIKA IBADA YA IJUMAA KUU Reviewed by By News Reporter on 4/20/2019 09:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.