Loading...

TRUMP ATISHIA MAHAKAMA YA KIMATAIFA ICC

Loading...
Rais wa Marekani Donald Trump aitolea vitisho mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita iwapo italenga kwa njia yeyote Israel au Marekani.

Wapalestina wameiomba mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita  kuanzisha uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu  uliotendwa na Israel.

Katika taarifa iliotolewa Ijumaa, rais wa Marekani amesema  Marekani itatoa jibu linalostahili iwapo mahakama hiyo italenga kwa njia yeyote  Marekani na mshirika wake Israel.

Mamlaka ya wapalestina  imeitaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kuanzisha uchunguzi dhidi ya Israel kwa ukiukwaji wake wa haki za binadamu dhidi ya wapalestina.

Kwa upande mwingine rais Trump  amepongeza kutupiliiwa mbali kwa uchunguzi uliotaka kuendeshwa dhidi ya wanajeshi wa Marekani kwa ukiukwaji wa haki na uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.

Muendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa mnamo mwaka 2017, alituhumu wanejeshi wa Marekani, majasusi wa CIA na wanamgambo wa kundi la Taliban kuwatesa wafungwa na  watuhumiwa kati ya mwaka 2003 na mwaka 2004 nchini Afghanistan.

Visa ya Bensouda kungia nchini Marekani  ilifutwa  wiki iliopita.

Ifahamike kuwa Marekani haikushiriki katika makubaliano yaliopelekea kusainiwa makubaliano ya Roma ambayo yaliafikiwa kuundwa kwa mahakama ya kimataifa.
Na Frank Kavikule.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TRUMP ATISHIA MAHAKAMA YA KIMATAIFA ICC TRUMP ATISHIA MAHAKAMA YA KIMATAIFA ICC Reviewed by By News Reporter on 4/14/2019 09:44:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.