Loading...

UGANDA: BOBI WINE ATOROKA KIZUIZINI, POLISI WAHAHA KUMSAKA

Loading...
Mbunge wa Kyadondo Mashriki Bobi Wine ameripotiwa kutoweka kusikojulikana siku moja baada ya maafisa wa polisi kumuweka kizuizini nyumbani kwake.

Bobi alikamatwa Jumatatu Aprili 22 alipokuwa akielekea eneo la Busabala ambapo alitarajiwa kuwahutubia wananchi. 

Kulingana na taarifa tulizozipokea hapa Dundiika News, mbunge huyo alitarajiwa kuzungumzia masuala kadhaa ikiwemo mauaji ya kiholela yanayotekelezwa na maafisa wa polisi na ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Hata hivyo, serikali kuu ilimkashifu Bobi kwa kukosa kuzingatia tahadhari za kiusalama alipoandaa halfa hiyo ya Kyarenga. 

Polisi waliokuwa wamezingira makazi ya mbunge huyo sasa wamepata kibarua cha kumsaka.
Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UGANDA: BOBI WINE ATOROKA KIZUIZINI, POLISI WAHAHA KUMSAKA UGANDA: BOBI WINE ATOROKA KIZUIZINI, POLISI WAHAHA KUMSAKA Reviewed by By News Reporter on 4/26/2019 09:04:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.