Loading...

WAKIMBIZI WADAI USALAMA WAO KAMBINI KIGOMA MASHAKANI

Loading...
Wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Nduta, Mkoani Kigoma wameiomba serikali ya Tanzania kuwahamisha kwenda kambi nyingine iliyoko mbali na eneo hilo ambalo liko mpakani na Burundi.

Wakimbizi hao wanadai kwamba kuna wahalifu kutoka Burundi wanaovuruga mara kwa mara usalama kambini humo na kwenye makazi ya Watanzania yalio jirani na kambi hiyo.

Madai yao ni kuwa hilo limepelekea wakimbizi katika kambi hiyo kushutumiwa kuwa wanahusika na uhalifu huo na baadae wao wanaadhibiwa kwa kurejeshwa Burundi, bila ya hiari yao.

Wakimbizi hao wa kambi ya Nduta wanasisitiza njia pekee ya kukomesha vitendo hivyo vya uhalifu katika kambi na mjini Kibondo ni kuwahamishia kwenda kambi nyingine mbali sana na mpakani, ndio muarubaini wa kukabiliana na wahalifu wanaovuka mpaka na kujipenyeza ndani ya kambi.

Wakimbizi wa Burundi karibu laki 4 walikimbilia katika nchi jirani kufwatia mgogoro wa kisiasa uliozuka mwezi April mwaka wa 2015 baada ya hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula mwengine wa tatu. Tanzania ndiyo ilipokea idadi kubwa ya wakimbizi. Kambi ya Nduta pekee inafifadhi Zaidi ya wakimbizi laki moja.
Na Frank Bernard.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAKIMBIZI WADAI USALAMA WAO KAMBINI KIGOMA MASHAKANI WAKIMBIZI WADAI USALAMA WAO KAMBINI KIGOMA MASHAKANI Reviewed by By News Reporter on 4/07/2019 09:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.