Loading...

AKAUNTI BILIONI TATU ZA WATUMIAJI MTANDAO WA FACEBOOK ZAFUNGWA, JE NI KWANINI? UFAFANUZI HUU HAPA

Loading...
Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019.

Katika kipindi hicho cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki - idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa.

Zaidi ya ujumbe milioni saba za"chuki" pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami.

Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina.

Akizungumza na vyombo vya habari mwanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg aliwakosoa vikali wale ambao wanatoa wito kampuni hiyo ivunjiliwe mbali, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuka.

"Sidhani suluhisho ni kuvunjilia mbali kampuni kwasababu tunashughulikia [tatizo hilo]," alisema.

"Ufanisi wa kampuni hii umetuwezesha kufadhili mpango huu kwa kiwango kikubwa. Kiwango cha fedha tunazotumia kuimarisha usalama wa mtandao wetu ni kikubwa kuliko ''mapato ya mwaka mzima'' ya mtandao wa Twiter.

Facebook imesema kumekuwa na ongezeko la akaunti bandia kwasababu "wahalifu" wamekuwa wakitumia mfumo maalum kuzifungua.

Lakini ikaongeza kuwa ilifanikiwa kuzigundua na kuzifuta zote katika kipindi cha dakika moja, kabla wapate nafasi ya kuzitumia kufanya "uhalifu ".

Mtando huo wa kijamii pia utaripoti ni posti zilizotolewa kwa kuuza "bidhaa ambazo zimedhibitiwa"kama vile bunduki na dawa.

Ilisema kuwa iliwachukilia hatua watumiaji milioni moja wa mtandao huo kwa kuuza bunduki katika miezi hiyo sita kipindi ambacho ilichukua kuaanda ripoti hiyo.

Ripoti hiyo pia ilikadiria idadi ya ujumbe, kama zile zinazoangazia unyanyasaji watoto, ghasia na propaganda kuhusu ugaidii,zinazowafikia wateja wake.
Na Zaina Philippo.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AKAUNTI BILIONI TATU ZA WATUMIAJI MTANDAO WA FACEBOOK ZAFUNGWA, JE NI KWANINI? UFAFANUZI HUU HAPA AKAUNTI BILIONI TATU ZA WATUMIAJI MTANDAO WA FACEBOOK ZAFUNGWA, JE NI KWANINI? UFAFANUZI HUU HAPA Reviewed by By News Reporter on 5/24/2019 09:24:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.