Loading...

SERIKALI YAONDOA TOZO 105 ZA MAZAO YA KILIMO

Loading...
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo, Obey Assery amesema mpaka sasa jumla ya tozo, ada na ushuru 105 zimeondolewa katika mazao ya kilimo.

Ossery ametoa kauli hiyo jana Mei 23, 2019 kupitia Mwananchi Jukwaa la Fikra linalofanyika Ukumbi wa Kisenga, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Amesema kufutwa kwa tozo hizo kulitokana na mikutano iliyowakutanisha wadau na kupata maoni yao kuwa ni kitu gani kinawapa kero na kinapaswa kuondolewa.

“Nyingine katika mbegu, viatilifu na mbolea, lakini pia tumerekebisha pia kanuni za mbolea katika kufanya majaribio kutoka Dola za Marekani 30,000 zlizokuwapo mwanzoni hadi kufikia Dola za Marekani 10,000,” amesema Ossery.

Mbali na hilo, pia amesema Wizara imeongeza muda wa vibali vya kusafirisha vyakula nje ya nchi hadi kufikia miezi miwili kutoka mwezi mmoja uliokuwa awali, lakini pia hupatikana kwa njia ya mtandao ili kupunguza muda wa kusubiri.

“Lakini hata tozo zetu, kodi na ushuru tunazikusanya kwa njia ya mtandao, hii imesaidia kuongeza mapato,” amesema Assery.
Na Daudi Mbuja.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SERIKALI YAONDOA TOZO 105 ZA MAZAO YA KILIMO SERIKALI YAONDOA TOZO 105 ZA MAZAO YA KILIMO Reviewed by By News Reporter on 5/24/2019 09:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.