Loading...

SAVIMBI KUZIKWA UPYA BAADA YA VIPIMO VYA DNA KUTHIBITISHA MABAKI YA MWILI WAKE

Loading...
Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Angola Jonas Savimbi, aliyeuawa mwaka 2002, unatarajiwa kuzikwa upya kijijini kwao Lopitanga mwezi ujao. 

Hii ni baada ya vipimo vya vinasaba (DNA) vilivyofanyika katika maabara za Afrika Kusini, Argentina, Ureno na Angola kuthibitisha kuwa mabaki hayo ni ya mwili wa Savimbi.

Kiongozi huyo wa waasi aliaga dunia wakati wa mapigano kati ya kundi lake na wanajeshi wa kikosi cha People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA) miaka 17 iliyopita, na alizikwa siku moja baadaye katika jimbo la Moxico lililopo mashariki mwa nchi hiyo. 

Taarifa iliyotolewa Jumatatu, Mei 20 na Waziri wa Nchi Pedro Sebastiao ilisemaza kuwa mazishi hayo yanaandaliwa baada ya vipimo kuthibitisha mwili uliochunguzwa ni wa Savimbi.

Wiki sita baada ya kuuawa na serikali ya kisoshalisti nchini humo Februari 22, 2002, kundi lake la Unita lilitia saini mkataba wa amani na majeshi ya serikali. 

Mgogoro kati ya vikosi vya Savimbi na serikali ulikuwa wa muda mrefu sana barani Afrika na makubaliano yaliyoafikiwa ya amani yalitatua mizozo huo uliozuka baada ya Angola kupata uhuru wake kutoka kwa Mreno mwaka 1975.
Na Richard Omondi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SAVIMBI KUZIKWA UPYA BAADA YA VIPIMO VYA DNA KUTHIBITISHA MABAKI YA MWILI WAKE SAVIMBI KUZIKWA UPYA BAADA YA VIPIMO VYA DNA KUTHIBITISHA MABAKI YA MWILI WAKE Reviewed by By News Reporter on 5/24/2019 09:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.