Loading...

SAKATA LA UCHAGUZI INDIA: MODI AWAACHA MIDOMO WAZI WAPINZANI KWA USHINDI MNONO

Loading...
Chama cha waziri mkuu wa India Narendra Modi kilikuwa njiani kurejea madarakani kwa kishindo baada ya kupata wingi mkubwa wa viti katika zoezi linaloendelea la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliodumu kwa wiki tatu.

Data rasmi kutoka tume ya uchaguzi zinaonyesha kuwa chama cha Modi cha Hindu - Nationalist Bharatiya Janata (BJP), kilikuwa mbele katika viti 298 kati ya viti 542 vinavyowaniwa.

Hili ni ongezeko kutoka viti 282 kilichopata chama hicho katika uchaguzi wa 2014, na zaidi ya viti 272 vinavyohitajika kupata wingi katika baraza la chini la bunge.

Chama kikuu cha upinzani cha Congress kilikuwa mbele katika viti 52 tu.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SAKATA LA UCHAGUZI INDIA: MODI AWAACHA MIDOMO WAZI WAPINZANI KWA USHINDI MNONO SAKATA LA UCHAGUZI INDIA: MODI AWAACHA MIDOMO WAZI WAPINZANI KWA USHINDI MNONO Reviewed by GEOFREY MASHEL on 5/24/2019 08:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.