Loading...

MO DEWJI KUTOA BODABODA KWA KILA MCHEZAJI WA SIMBA KWA KUBEBA KOMBE

Loading...
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi klabu ya Simba, Mohammed Dewji amehaidi kuwapa pikipiki aina Boxer yenye thamani ya Sh 2.4 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Dewji alisema hayo wakati wa kuipongeza timu hiyo kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na zawadi hiyo imetoka kutoka kwake mwenyewe.

Alisema kuwa amewaomba wachezaji kutumia pikipiki hizo kama kitega uchumi na kuwapa ndugu zao ili kujiingizia kipato kila siku.

Alisema kuwa wanaweza kuingia mkataba na ndugu zao ambao hawana kazi na kujipatia sh 15,000 kwa siku mpaka hapo mkataba utakapo malizika.

“Nimefarijika kwa mafanikio ya timu ambayo yametokana na umoja wa ndani ya klabu baada ya kuanza mfumo mpya wa uongozi,” alisema Dewji.

Alisema kuwa zawadi hiyo itawajenga wachezaji na kuona tija kwa kazi waliyoifanya katika ligi kuu ya Tanzania Bara.
Na Ummy Zuberi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MO DEWJI KUTOA BODABODA KWA KILA MCHEZAJI WA SIMBA KWA KUBEBA KOMBE MO DEWJI KUTOA BODABODA KWA KILA MCHEZAJI WA SIMBA KWA KUBEBA KOMBE Reviewed by By News Reporter on 5/23/2019 08:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.