Loading...

FIFA KUBAKIZA TIMU 32 ZILE ZILE, WASITISHA MPANGO WA TIMU 48

Loading...
Shirikisho la Soka Duniani Fifa limesitisha mpango wa kuongeza nchi zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 hadi timu 48.

Rais wa Fifa Gianni Infantino mwaka jana alisema mpango wa kuongeza timu hizo kutoka 32 ambao ungelianza kutekelezwa mwaka 2026 urudishwe nyuma hadi mwaka 2022.

Mabadiliko hayo yalimaanisha Qatar ambayo ndio mwandalizi wa mashindano hayo kushirikiana na mataifa mengine katika kanda hiyo.

Shirikisho hilo lilisema "baada ya mashauriano ya kina" tumeonelea mabadiliko hayo "hayawezi kutekelezwa kama ilivyopangwa awali".

Fifa pia imesema ilitathmini uwezewkano wa Qatar kuandaa peke yake mashindano hayo ikiwa na timu 48 lakini ikaamua kusitisha mpango huo kutokana na changamoto ya ukosefu wa muda wa kutosha wa "kufanya ukaguzi wa kubaini athari ya hatua hiyo, matokeo yake na jinsi ya kushughulikia masuala ibuka ".
Na Rehema Daudi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FIFA KUBAKIZA TIMU 32 ZILE ZILE, WASITISHA MPANGO WA TIMU 48 FIFA KUBAKIZA TIMU 32 ZILE ZILE, WASITISHA MPANGO WA TIMU 48 Reviewed by By News Reporter on 5/23/2019 08:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.