Loading...

BOTSWANA TEMBO KUWINDWA KAMA SWALA, WANAHARAKATI WANYAMA WADODOSA NENO

Loading...
Botswana imeondoa marufuku ya uwindaji tembo kutokana na ongezeko la mzozo kati ya binadamu na wanyama ambao wanaharibu mashamba yao.

Wakosoaji wa marufuku hiyo iliyowekwa mwaka 2014, wanasema udhibiti huo ulikuwa unawaathiri wakulima wadogo na watu waliyokua wakinufaika na uwindaji wa mnyama huyo.

Hatua hiyo huenda ikakosolewa vikali na wanaharakati wa uhifadhi wa wanyama ambao wanaamini imetokana na sababu za kisiasa.

Kuna hofu uamuzi huo utaathiri sifa ya nchi hiyo kimataifa hali ambayo pia huenda ikaathiri mapato yanayotokana na utalii ambao ni chanzo kikubwa cha mapato ya kifeni kwa taifa hilo baada ya uchimbaji madini ya Almasi.

WATAALAMU WA UHIFADHI WANASEMA NINI?

Wataalamu wa uhifadhi wanasema mbuga za wanyama zinakabiliwa na changamoto za kiekolojia kwasababu wanyama wamekua wengi kupita kiasi katika hifadhi zao, maji yamekua haba na malisho au chakula chao pia kimepungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Utafiti unaonesha kuwa tembo wanasafiri mbali na umbali wa safari zao umeendelea kuongezeka.

Tembo wanaweza kusababisha uharibifu mkubwa wanapovamia mashamba na wakati mwingine wanaweza kuua watu wakijaribu kuwafukuza.

Idadi kubwa ya tembo nchini Botswana wanapatikana katika maeneo ya mpaka wa Namibia, Zambia na Zimbabwe.

Wanaharakati wa kimataifa wa uhifadhi wamekuwa wakishinikiza marufuku ya uwindaji tembo kama njia ya kukabiliana na uwindaji haramu.
Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BOTSWANA TEMBO KUWINDWA KAMA SWALA, WANAHARAKATI WANYAMA WADODOSA NENO BOTSWANA TEMBO KUWINDWA KAMA SWALA, WANAHARAKATI WANYAMA WADODOSA NENO Reviewed by By News Reporter on 5/23/2019 08:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.