Loading...

BABAKE RAIS WA CONGO KUZIKWA KISHUJAA, MWILI WAKE KUWASILI LEO - DRC

Loading...
Mwili wa kiongozi wa Upinzani ambaye pia ni babake rais wa DR Congo utawasili nchini humo yapata miaka miwili baada ya kifo chake nchini Ubelgiji kulingana na familia yake.

Etienne Tshisekedi ambaye mwanawe Felix aliapishwa kuwa rais wa taifa hilo atawasili nchini humo kwa mazishi.

Alifariki mjini Brussels akiwa na umri wa miaka 84 mnamo mwezi februari 2017 lakini mwili wake ulisalia katika mji huo wa Ubelgiji kutokana na wasiwasi wa kisiasa na utawala wa rais wa zamani wa taifa hilo Josep kabila.

Mwili wa Etienne Tshisekedi utawasili tarehe 30 na mazishi yake yatafanyika katika uwanja wa Martyrs Stadium , kulingana na nduguye Askofu Gerard Mulumba.

Mulumba anasema kuwa baada ya kuukaribisha mwili katika uwanja wa ndege , uatasafirishwa hadi katika uwanja huo kwa maombolezi .

Amesema kuwa tayari maandalizi katika uwanja huo ikiwemo ujenzi wa jukwaa umekamilika mbali na yale ya maafisa wa polisi ambao wataongoza gwaride ili kumpatia heshima za mwisho baba huyo wa upinzani.

Uwanja huo wa Martyrs unabeba zaidi ya raia 80. Takriban marais watano wa bara la Afrika wamethibitisha kuhudhuria mazishi yake.

Amesema kuwa mazishi yake yatafanyika mjini Kinshasa lakini kabla ya hapo mwili wake utapitishwa katia jumba la Chama na baadaye upelekwe nyumbani kwake kabla ya kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Baadaye siku inayofuata itakuwa ya sherehe na Misa.

''Katika siku ya sita maandalizi ya mwisho ya kumuaga mzee na baadaye kumstiri yatafanyika'', aliongezea.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BABAKE RAIS WA CONGO KUZIKWA KISHUJAA, MWILI WAKE KUWASILI LEO - DRC BABAKE RAIS WA CONGO KUZIKWA KISHUJAA, MWILI WAKE KUWASILI LEO - DRC Reviewed by By News Reporter on 5/30/2019 07:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.