Loading...

FAHAMU FAIDA ZA TENDE HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MFUNGO WA RAMADHANI

Loading...
Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipee.

Zifuatazo ni faida ya tunda la tende katika mwili wa binadamu:-

Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina.

Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.

Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FAHAMU FAIDA ZA TENDE HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MFUNGO WA RAMADHANI FAHAMU FAIDA ZA TENDE HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MFUNGO WA RAMADHANI Reviewed by By News Reporter on 5/13/2019 07:51:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.