Loading...

UNENE KUPITA KIASI HUONGEZA HATARI KIFO CHA MAPEMA

Loading...
Watafiti nchini Uingereza wamegundua kwamba kiribatumbo huongeza hatari ya kifo cha mapema

Kiribatumbo (unene kupita kiasi) huongeza hatari ya kifo cha mapema kwa asilimia 50.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na SkyNews, Nchini Uingereza umefanywa utafiti wa afya na sababu za vifo kwa watu milioni 2.8. Katika utafiti huo wataalamu wamegundua kwamba  hatari ya kufa mapema kwa watu wenye BMI ( kipimo cha unene) kati ya 40 na 45 huongezeka kwa asilimia 50.

Watu wanene ambao kilo zao zinawiana na kiwango hicho cha BMI pia hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari huongezeka mara 12. Hatari ya kukosa hewa wakiwa usinginzini huongezeka mara 22. Hatari ya kupata matatizo ya moya, shinikizo la damu na ongezeko la mafuta katika damu huongezeka mara 3.

Hata kwa watu wanene ambao wenye uzito sawa na BMI 25 na 30 bado hatari ya kupata magonjwa ya moyo huongezeka kwa asilimia 20.

Matokeo ya utafiti huu yametolewa katika kongamano la kiribatumbo barani Ulaya yaliyofanyika Glasgow.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UNENE KUPITA KIASI HUONGEZA HATARI KIFO CHA MAPEMA UNENE KUPITA KIASI HUONGEZA HATARI KIFO CHA MAPEMA Reviewed by By News Reporter on 5/13/2019 08:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.