Loading...

"WISE HONEST" MELI YA KOREA KASKAZINI ILIYOTEKWA NYARA NA MAREKANI

Loading...
“Wise Honest” meli ya mizigo ya Korea kaskazini iliyokuwa imebeba makaa ya mawe ambayo katikati ya wiki Marekani ilitangaza kuikamata katika kama hitajio la vikwazo vya kimataifa, imefika katika bahari ya Pasifik eneo la Samoa ya Amerika.

Kiongozi wa mahusiano ya jamii wa kikosi cha usalama wa pwani za Marekani, Amanda Wyrick amesema Wise Honest imeweka nanga katika mji mkuu wa Samoa ya Amerika, Pago Pago na kwamba uchunguzi wote juu ya meli hio utafanyika hapo.

Wyrick alisema meli hiyo haita toka hapo Samoa kwenda mahali popote mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Wizara ya sharia ya Marekani ilitangaza kuikamata meli ya Korea kaskazini iliyokuwa imebeba makaa yam awe kwa kuwa meli hio ilikuwa imekaribia eneo la bahari la nchi hio.

Ni mara ya kwanza kwa Marekani kukamata meli ya Korea kaskazini. Imesemwa kwamba meli hiyo ilisogelea pwani za Marekani kwa bahati mbaya kwa kuwa ilikuwa ikihitaji vifaa na matengenezo.

Katika taarifa iliyotolewa imeelzwa kwamba kwa kusafirisha makaa yam awe kuelekea Korea kaskazini, meli hiyo imevunjwa vikwazo vya kimataifa.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
"WISE HONEST" MELI YA KOREA KASKAZINI ILIYOTEKWA NYARA NA MAREKANI "WISE HONEST" MELI YA KOREA KASKAZINI ILIYOTEKWA NYARA NA MAREKANI Reviewed by By News Reporter on 5/13/2019 08:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.