Loading...

KUNDI LA ISLAMIC STATE NA ADF KUUNGANA KUTEKELEZA UGAIDI MASHARIKI MWA DRC

Loading...
Wakuu wa vyombo vya usalama katika kanda ya Maziwa Makuu wanakutana nchini Uganda kupanga mikakati ya kukabiliana na tishio la kundi la Islamic State ambalo linasemekana limeanza kuendesha harakati zake katika maeneo ya Mashariki na Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hayo ni kwa mujibu wa upelelezi wa chombo cha usalama kinachowaleta pamoja wakuu wa usalama katika kanda ya maziwa makuu, kuna uwezekano wa eneo hilo kuingiliwa kirahisi na wanamgambo wa kundi hilo kutokana na ukosefu wa usalama na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao unatatiza juhudi za kukabiliana nao.

Vyombo vya usalama katika eneo hilo sasa vinataka kuhakikisha kuwa kundi hilo halipati nafasi kuendesha shughuli zake katika mataifa ya eneo hilo baada ya kutimuliwa mashariki ya kati.

''Kuna vitisho kwa hivyo ni onyo kwetu kulishughulika mapema kabla halijawa tatiza kubwa katika kanda ya maziwa makuu'' alisema Mkuu wa Jeshi la Uganda, Jenerali David Muhoozi'

Kulingana na wakuu hao wa usalama kuna haja ya wao kushirikiana na majeshi ya mataifa ya kigeni yaliyochangia katika juhudi za kuvunja kundi hilo mashariki ya kati.

''Tishio la kundi hilo la kigaidi ni kubwa kiasi ya kuhamasisha Serikali za eneo hili lote la Maziwa Makuu, kuona ya kwamba zinaongeza juhudi za kukabiliana masuala ya kigaidi iwe ni kutoka kwa kundi la al-Shabab, ISIS, Boko Haram au Al-Qaeda'', alisema katibu mtendaji wa mataifa ya maziwa makuu, Zakaria Mubuli Mwita.

Aliongeza kuwa wamepokea ripoti kutoka kwa serikali za eneo hilo kwamba kundi la kigaidi la ADF linashirikiana na na makundi hayo ya kigaidi.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KUNDI LA ISLAMIC STATE NA ADF KUUNGANA KUTEKELEZA UGAIDI MASHARIKI MWA DRC KUNDI LA ISLAMIC STATE NA ADF KUUNGANA KUTEKELEZA UGAIDI MASHARIKI MWA DRC Reviewed by By News Reporter on 5/23/2019 08:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.